Saturday, May 15, 2004

Nakusikia Dada Hidaya

nakusikia dada hidaya
huku ughaibuni kuna mema na mabaya
wabeberu hawakosi njama za kuhujumu vibaya
watu wote wanaopinga sera zao mbaya mbaya
lakini nisikize dadangu hidaya


siwezi kamwe kunyamaza kimya
kama bubu mwenye bumbwazi
lazima tuseme wazi wazi
kwamba hawa mabepari wavamizi
ni majambazi matapeli na walanguzi

propaganda zao tumekataa
kutoka uganda kupitia qatar
hata kufikia kote ulimwenguni

dada hidaya nakudokezea hivi
wapende wasipende tumekataa kata kata
kudanganywa ni warongo kama akina christiani amampouri na mwolf mbwa mwitu mbweha mblitzer
watake wasitake hatutashangilia kamwe
watoto na wanawake wa baghdad wakichinjwa kama wanyama
na mafisi manguruwe wavamizi kutoka magharibi

kesho pengine watajigamba
kwamba wameshinda
watajifanya kwamba eti ni wakombozi

lakini sote twajua
katika vita dhidi ya wakoloni mamboleo
mapambano yataendelea
miaka nenda rudi
mpaka mwamerika na kibaraka chake mwingereza
kutimuliwa na ndugu zetu wazalendo wa kiarabu wa irak
na taifa zingine huko mashariki ya kati

hivyo hivyo nakushukuru dada hidaya
kwa maneno yako za hekima ya kunitakia mema

basi baadaye tuwasiliane dada hidaya
ni mimi nduguyo onyango oloo
nikishikilia pale pale
hapa jijini montreal
mkoani quebec
nchini canada
barani amerika kaskazini

ni saa nne inatimia
na mimi nitakomea hapa
kwa siku hii ya leo
tarehe saba mwezi wa nne
mwaka wa elfu mbili na tatu