Saturday, May 15, 2004

Zinduka

zinduka
nyanyuka
amka

zinduka upambane
amka na utamke
inuka na uchangamke

leo ni leo
tizama
kumepambazuka
angalia
kumekucha

wakati umewadia
hapa kwetu
kenya
wenzetu wakenya
kipindi kimefika
majira ya mabadiliko
na mapinduzi

ni wakati wa kutafutana na kupatana
wakati wa kushikamana na kuungana
mimi nanena nikisema
mwananchi zinduka

mimi nasema
mzalendo nyanyuka
zinduka
nyanyuka
amka
zinduka upambane
zinduka upambane

inuka
changamka
tamka
pambana usiku na mchana
pambana kufa na kupona
mpaka sisi sote tupate ushindi

tumechokeshwa na udhalimu
tunadhalilishwa na ufisadi
tumemaskinishwa na uporaji
tumeghadhabishwa na usaliti
wahenga walinena
mwizi ana siku arobaini
wakenya leo wanasema
wezi wa kanu wamemaliza miaka arobaini
wakishikilia kwa nguvu hatamu za uongozi

kabla sijafika kikomo nina maswali

nyumba hii yetu tuisafishe ama tuibomoe?
nyumba hii yetu tuifagie ama tuijenge upya?